TUTAWAFUNGA SIMBA KWA TAHADHARI….HUWA WANAPANIA SANA MECHI HII…
KOCHA Mkuu wa Yanga , Miguel Gamondi ameonekana bado anahitaji kuwa makini mbele ya Simba kwa kutumia muda wa kutazama michezo yote mikubwa waliocheza wapinzani wao hivi karibuni. Hatua hiyo kuelekea katika mchezo wa Kariakoo Derby dhidi ya Wekundu wa Msimbazi hao kwa kuhitaji msimu huu kuvuna alama zote sita zile za mzunguko wa kwanza walizoshida bao 5-1 na Jumamosi hii kutafuta ushindi. Yanga watakuwa wenyeji ikiwakaribisha Simba mchezo huo utakaochezwa Jumamosi hii katika dimba la Benjamin Mkapa Dar es Salaam, saa 11:00 jioni. Kocha huyo ameamua kukaa na wachezaji kupitia michezo mbalimbali ili kuweza kila mmoja anawezaje kufanya majukumu yake. Kwa mujibu wa Gamondi kuwa licha ya Simba kutokuwa vizuri hivi karibuni lakini mpinzani wake huyo amekuwa hatari hasa katika mechi kubwa na kumlazimi kuanza kufatilia na kuona ubora wao. Amesema ameona uimara wa safu ya ushambuliaji, viungo na ulinzi kwa wapinzani wake ikiwrmo kwenye upigaji wa mipira ya vichwa na kutakiwa kufanyia kazi kil